Kwa sasa Tanzania ishu ambayo inazikamata headline kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni ishu ya serikali kuhamia Dodoma. Ripota wa millardayo.com na AyoTV amefika kuzungumza na Serikali ya mkoa wa Dodoma na amezungumza na Katibu tawala wa mkoa wa Dodoma Rehema Seif Madenge ambapo ameainisha mambo mbalimbali yaliyopo kwenye mpango kazi wa kuhamia Dodoma……
- Tuliainisha majengo na maeneo ambayo yanaweza kutumika kama ofisi na pia majengo yatakayotumika kama makazi ili pale watakapoanza kuhamia tufahamu kiasi gani serikali inaweza kuhamia Dodoma.
- Tuliangalia na tukapendekeza kwamba serikali ianze kuhamia kwa awamu
- Tuliangalia shule zetu za msingi na sekondari zinaweza kupokea kiasi gani cha wanafunzi lakini pia masuala ya afya, vituo vyetu vya afya zahanati zetu zitaweza kupokea watu kiasi gani.
- Miundombinu ya barabara kwamba barabara zetu zinaweza kupokea kiasi gani cha magari lakini tunapendekeza kuwe na taa za barabarani, mitaa iwe na majina na anuani za makazi ili iwe rahisi kufanya mawasiliano.
- Tuliangalia kwa namna gani eneo ambalo mji wa serikali utajengwa, katika hilo tunapendekeza kwamba mji wa serikali uwe nje ya hapa katikati Dodoma ili kuondokana na hali iliyopo kule Dar es salaam.
- Tunapendekeza pia ule mji wa serikali usiwe mahali pamoja
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
YAKUFAHAMU KUHUSU GHARAMA ZA KUPANGA NYUMBA NA KUNUNUA VIWANJA DODOMA, UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI