Vikao vya bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017 ambalo limemalizika hivi karibuni huku ikishuhudiwa wabunge wanaounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, wakitoka nje na kutohudhuria vikao hivyo.
Leo August 21 2016 kupitia kipindi cha funguka kinachorushwa na kituo cha television cha Azam Tv, mbunge wa Vunjo na mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia ameizungumzia kauli iliyotolewa na Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa anakusudia kuletafuta maridhiano baina ya wabunge wanaounda umoja wa katiba, UKAWA na naibu Spika, Mbatia amesema……….
>>>’Kauli ya Spika Ndugai ni kauli yenye kuleta matumaini kwa sababu sisi ndani ya wabunge wa upinzani tulichokuwa tunazungumza na tulitafuta nafasi hizo, fursa hizo tuliweza kuwaende hata wenzetu wa upande mwingine kuwa sisi ni watu wa maridhiano’
ULIKOSA HII YA MBATIA KUSEMA KUWA HATUKUSUSIA BUNGE KWA AJILI YA MTU MMOJA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI