Teknolojia kila kukicha inazidi kuchukua headlines mtu wangu ili kuweza kurahisisha mambo mbalimbali, wakati napitapita zangu katika moja kati ya restaurant za Lubumbashi DRC Congo nikisubiri mchezo wa TP Mazembe dhidi ya Yanga, nimekutana na teknolojia inayotumika katika restauranta za Lubumbashi.
Tofauti na ilivyo kwa baadhi ya restaurant kubwa za Dar es Salaam ambapo kama una oda ya chakula kwa ajili ya kula au kuondoka nacho lazima usubirie karibu na counter au ukae sehemu na kumuonesha muhudu ulipo ili chakula chako kikiwa tayari akuletee, Lubumbashi katika restaurant zao wanakifaa maalum cha kusaidia kazi hiyo.
Kama umeoda chakula kwa Lubumbashi unaweza kwenda kukaa eneo lolote ndani ya restaurant au hata nje maeneo jirani ya hapo pasipo muhudumu kujua ulipo, lakini kifaa ulichopewa chakula chako kikiwa tayari kinapiga alarm na kuwaka taa kuashiria kuwa urudi counter kwa ajili ya kuchukua chakula chako.
Angalia video ya kifaa chenyewe ambacho kinatumika katika restauranza Lubumbashi kama Carrefour Food Court
Kama uliikosa mipango ya Dodoma kuwa na Mlimani City yao na barabara za juu