August 23 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka Mabalozi wanne wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi hao ni Roberto Mengoni -Balozi wa Italia hapa nchini, Kim Yong Su – Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini, Mohamed Hassan Abdi – Balozi wa Jamhuri ya Somalia hapa nchini na Paul Sherlock – Balozi wa Ireland hapa nchini.
Akizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati za utambulisho za Mabalozi hao Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itawapa ushirikiano wa kutosha ili kuendeleza na kuuimarisha zaidi uhusiano ulipo kati ya nchi hizo na Tanzania.
Dkt. Magufuli amewaambia Mabalozi hao kuwa katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 Tanzania imedhamiria kutekeleza mpango wa ujenzi wa viwanda, hivyo amezialika nchi zao na sekta binafsi katika nchi hizo kuungana na Tanzania katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda na biashara.
Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ireland Paul Sherlock alisema…….>>>“Naomba kukuhakikishia kuwa Wafanyabiashara watakaokuja kuwekeza ama kufanya biashara, mitaji yao itakuwa salama na Serikali yangu itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha uwekezaji huo unafanikiwa na unanufaisha pande zote mbili”
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUTHIBITISHA KUYAPIGA MNADA MAJENGO YA SERIKALI UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI