Michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi kwa upande wa wawakilishi pekee wa Tanzania klabu ya Dar es Salaam Young Africans imemalizika leo August 23 2016, kwa Yanga kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya TP Mazembe katika uwanja wa Stade TP Mazembe Lubumbashi DRC Congo.
Yanga ambao walikuwa ugenini na pungufu kwa kuwakosa mabeki wao mahiri katika safu ya ulinzi, wamekubali kipigo cha goli 3-1 kutoka kwa wenyeji wao TP Mazembe, Yanga walianza kuruhusu goli la kwanza dakika ya 28 baada ya Jonathan Bolingi Mpangi na Rainford Kalaba akapachika goli mbili dakika ya 55 na 64, Dakika ya 78 Yanga walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Amissi Tambwe aliyemalizia mpira wa faulo uliyogonga nguzo ya goli.
Kwa sasa Yanga wanakuwa wamemaliza michuano hiyo ya Kombe la shirikisho barani Afrika wakiwa na point nne na kuambulia kushika mkia katika msimamo wa Kundi A lililokuwa na timu za TP Mazembe ya Congo, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, waliofuzu hatua ya nusu fainali ni vinara TP Mazembe wenye point 13 na Medeama wenye point nane na wamefuzu kwa tofauti ya magoli dhidi ya MO Bejaia.
GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1