Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya August 24 2016 ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Wenye VVU sasa kuwahishiwa ARVs’
#NIPASHE Watakaogundulika kuwa na VVU kuanza dawa papo hapo badala ya kusubiri mpaka kinga za mwili kupungua pic.twitter.com/BJtj0mXVsp
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
Watu watakaogundulika kuwa na virusi vya Ukimwi (VVU) wataanza kupewa na kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa (ARVs) bila kusubiri kinga zao za mwili kupungua kama ilivyozoeleka.
Wakati utaratibu huo mpya ukitarajiwa kuanza october mwaka huu, kwa upande wake Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kupitia kwa Mwenyekiti wake Constantine Kanyasu, imeshauri serikali kuangalia namna ya kuruhusu dawa ziingizwe na kuuzwa madukani kwa bei nafuu ka ajili ya watu ambao hawako chini ya mpango wa serikali.
Hayo yameelezwa jana mjini Dodoma kwenye kikao cha kamati hiyo ya Bunge ambayo ilipokea taarifa iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulusubisya alielezea kamati juu ya mabadiliko katika tiba na kusema mtu yeyote anayepima na kugundulika kuwa na Virusi vya Ukimwi, ataanza kupatiwa ARVs mara moja.
Source: HabariLeo
Unaweza kupitia hapa habari nyingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania August 24 2016
#NIPASHE 316 waliokatishwa masomo St. Joseph wameifikisha mahakamani TCU na chuo hicho wataka kulipwa zaidi ya bil 5 pic.twitter.com/UKRIvAFKTU
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#NIPASHE Mke wa bilionea Msuya afikishwa mahakama ya Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya dada wa Msuya pic.twitter.com/AoVSMhgtEP
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#MWANANCHI Mkutano CUF uliojadili ajenda ya kupitisha barua ya kujiuzulu Lipumba ulitumia mil 500 kwa maandalizi pic.twitter.com/8DxSfvmmqc
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#MWANANCHI Polisi wazuia msafara wa Lowassa kuingia Rukwa kwa maelezo unaweza kuingilia ziara ya waziri mkuu pic.twitter.com/O39Wa5OxWY
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#MWANANCHI Abiria wasiojiweza JNIA wabebwa kwa machela kutokana na ubovu wa lifti za uwanja huo pic.twitter.com/09M5PpnfPi
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#MWANANCHI Waziri Ummy aishauri Aga Khan kujenga hospitali Dodoma ili kupanua huduma zake pic.twitter.com/B30Bugc7Od
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#MWANANCHI Waziri Ndalichako ataka bil 12 za utafiti zitumike kutatua matatizo ya wananchi pic.twitter.com/UJWJVRHEy4
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#MTANZANIA Muhimbili kununua helcopter itakayokuwa inasafirisha wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali hadi hospitalini pic.twitter.com/6SSyKmOwdS
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#MTANZANIA Uongozi shule ya sekondari Mwasiti wilaya ya Rungwe Mbeya umemfukuza mwanafunzi kwa madai ya ushirikina pic.twitter.com/eESp8W0i6n
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#UHURU Kampuni ya tumbaku TLTC yafungiwa kutokana na kukaidi maagizo ya serikali ya kulipa fedha za wakulima pic.twitter.com/lXIt9D1IMe
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#NIPASHE TRL imeongeza treni moja na kufikisha tatu ktk safari za mikoani, itakuwa inaondoka DSM kila jumapili pic.twitter.com/ilm4EqN5N8
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
#NIPASHE Kamati ya bunge ya miundombinu imeiagiza TAMESA kujiendesha na serikali ilipe deni la zaidi ya bil 13 pic.twitter.com/29huDgaU9E
— millardayo (@millardayo) August 24, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV AUGUST 24 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI