Usiku wa August 23 2016 moja ya tukio lililotawala katika baadhi ya mitandao ya kijamii ni pamoja na kuuwawa kwa Askari Polisi wanne Mbande nje kidogo ya Dar es salaam baada ya majambazi kuvamia eneo lililokaribu na Bank ya CRDB.
Ayo TV ilimpata mmoja wa majeruhi katika shambulio hilo anayefahamika kwa jina la Ally Kiyonda ambaye ni raia wa kawaida anasema…>>>’Walikuja majambazi wakiwa na pikipiki kama tano wakiwa wamepakizana huku kila mmoja akiwa na bunduki yake‘
‘Walivyofika walionyeshea silaha zao eneo la bank ya CRDB na baadae wakaanza kupiga risasi upande wetu hivyo moja ikanipiga katika mguu‘ –Ally Kiyonda
Unaweza kuendelea kumsikiliza na kumtazama kwenye hii video hapa chini…
ULIIKOSA ALICHOKIONGEA WAZIRI NCHEMBA BAADA YA MAUAJI YA POLISI KUTOKEA DAR