Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 24 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel 10
GEGODETA yapinga operesheni ukuta, mwenyekiti wa tasisi hiyo ya Geogeta Thomas Ngawaiya ameyazingumzia haya kuhusiana na ukuta
>>>’Wananchi wote twende mbele hatutakwenda mbele kwa maandamano, kama kuna tatizo watu wakae mezani wajadili ‘- Mwenyekiti Geogeta, Thomas Ngawaiya
Habari kutoka Clouds TV
Ujenzi wa hospitali Chanika, Hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 160 na itakuwa na nyumba za kuishi madaktari na familia 28,pia itakuwa na chuo cha kutoa mafunzo maalum ya afya. Ujenzi wa hospitali hiyo utagharimu zaidi ya shillingi Billioni 8.8 ambapo ujenzi wake unataraji kumalizika March 2017.
Habari kutoka ITV
Uvuvi Haramu
Zana haramu za uvuvi zimekamatwa katika maeneo mbalimbali Kagera, Informer wa mkoa huo waonywa wasifanye hii kitu wanatakiwa wawe mbele kusimamia na kutokomeza uhalifu huu wa uvuvi kwahiyo wasiwe sehemu ya tatizo hili, tunawaonya sana na atakae bainika tutamchukulia hatua kali za kisheria .
Habari kutoka Azam TWO
Diaspora tushiriki kupiga kura
>>> ‘Zile logistics za kupiga kura tukiwa mbali na kusafirisha zile kura na kujumulishwa kwenye kamati ya kura nadhani ni moja ya matatizo, sio kwamba serikali haitaki watanzania washiriki lakini tutafute utaratibu na mimi natoa wito kwa independent commissions ya mainland na ya Zanzibar tutafute namna ya kushiriki wananchi walio nje na walio halali katika kupiga kura za uchaguzi mkuu au uchaguzi wa serikali za mitaa‘ –waziri wa mambo ya nje na ushirikiano Afrika mashariki, Augustine Mahiga
Habari kutoka Channel Ten
Maandamano ya ukuta September mosi
‘ Tuwe na hakika amani tunayodai kwamba ni muhimu sana tunaombea watu waiombee itatuponyoka, tusisahau ya Zanzibar’ – Kingunge Ngombale Mwiru
ULIKOSA KUITAZAMA VIDEO YA TAARIFA KUHUSU MIKUTANO YA SIASA NCHINI? UNAWEZA KUITAZAMA NIMEKUWEKEA HAPA CHINI