Siku ya kwanza ya mwezi September 2016 imekua ikitajwa sana kwenye headlines siku za karibuni na ni baada ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano nchi nzima, maandamano ambayo hata hivyo vyombo vya dola viliyapiga marufuku.
Baada ya vichwa vyote vya habari na kwamba siku hii Jeshi la Wananchi wa Tanzania limeamua kuitumia kuadhimisha miaka yake 52, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe leo August 31 mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam ameyasema yafuatayo.
>> ‘Tunaahirisha mikutano, maandamano UKUTA kwa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka-Mbowe‘ – Freeman Mbowe
‘Tunaahirisha mikutano, maandamano UKUTA kwa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka-Mbowe pic.twitter.com/TmpjsZZYiZ
— millard ayo (@millardayo) August 31, 2016
.
‘Viongozi wa dini walituambia tupeni wiki mbili au tatu, sisi tukawaongeza nyingine moja’-Mbowe pic.twitter.com/Y8d0eJdnNS
— millard ayo (@millardayo) August 31, 2016
.
‘Wadau walitusihi tusitishe ila tusiache, tumepata wakati mgumu mno kufikia uamuzi huu’-Mbowe pic.twitter.com/2evQCTLVWI
— millard ayo (@millardayo) August 31, 2016
ULIKOSA KUONA ALICHOSEMA MKUU WA MKOA DSM KUHUSU SEPTEMBER 1 2016 ? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI