Jitihada za BancABC katika ubunifu kuendeleza na kufanikisha usalama wa miamala matandaoni Tanzania imetambuliwa kwa tuzo ya ViISA kuthibitisha ubora wa huduma yake mitandaoni.
Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na wafanyabishara wadogo Joyce Malai alithibitisha taarifa hiyo alipozungumza na vyombo vya habari mapema katika makao makuu ya bank ABC Dar es salaam.
“Tunafurahi kupokea tuzo hii licha ya ushindani wa masoko uliopo, hii inaonyesha ni jinsi gani tumejidhatiti kuhudumia wateja wetu na kuwarahisishia kufanya miamala ya kifedha,” alisema Bi. Malai.
Akasema tena kwamba katika jitihada hizi za kuboresha miamala salama mitandaoni, mtu yeyote anaweza kumiliki kadi hii ya VISA bila kujali kama anayo akaunti ya BancABC au la.
Bi. Malai alifafanua kwamba kadi ya VISA ya BancABC ni rahisi kutumia kwani inamuhakikishia mteja ulinzi wa fedha zake na pia huondoa usumbufu wa kutembea na pesa taslimu.
Kadi hii inaweza kutumika kufanyia miamala mbalimbali ya kifedha kama vile kulipia tiketi za ndege pia kulipa posho na mishahara kwa wafanyakazi, kulipa ada za shule na kujikimu kwa wanafunzi, mikopo na misaada kwa serikali na mengineyo.
Sasa kama hapo ulipo upo tayari kuichukua hii kadi unatakiwa kwenda na kitambulisho halisi na kisha kujaza fomu zinazopatikana katika tawi lolote la benki hii.
Wateja wanaweza kuweka fedha kwenye kadi hii kwa kutumia huduma mbalimbali za kutuma pesa kama vile TIGOPESA, AIRTELMONEY au M-PESA pamoja na benki nyingine zilizopo Tanzania.