Kumekuwa na headline za kwamba hivi sasa serikali ya Tanzania inadaiwa deni la taifa zaidi ya trilion 51 ambazo katika mgawanyo inaonyesha kwamba kila mtanzania atatakiwa kulilipa deni hilo, ishu imefikishwa hadi bungeni leo ambapo mbunge wa Hai Freeman Mbowe alitaka ufafanuzi wa jambo hili kutoka serikalini.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba alisimama kumjibu Mbowe…>>>’Kwanza hakuna siku watanzania watagongewa milango wakigawanywa deni hilo la taifa, hakuna utaratibu wa taifa lolote kupima deni kwa kuangalia ujazo wa watu‘ -Waziri Nchemba
‘Lazima mjue kwamba serikali huwa haikopi kwa ajili ya matumizi ya kawaida bali serikali hukopa kwa ajili ya maendeleo ambayo itazalisha na kulipa deni hilo’ –Waziri Nchemba
Video yote nimekuwekea hapa chini..
ULIMIS HAYA MATATU YA WAZIRI NCHEMBA KUHUSU CHANGAMOTO ZA ASKARI