Kila siku ya alhamis katika vikao vya bunge huanza kwa kipengele cha maswali na majibu ya wabunge kwenda kwa Waziri mkuu wa serikali ya Tanzania, leo September 8 2016 utaratibu huo uliendelea ambapo hapa nimekusogezea baadhi ya sentensi za Waziri mkuu Kassim Majaliwa ikiwa ni pamoja na matukio ya mauaji ya askari na raia wa kawaida.
'Kupungua kwa mizigo bandarini kumekuwa kukizungumziwa, serikali tunamkakati wa kuliangalia hilo ili kulinda uchumi #Waziri_mkuu_Majaliwa
— millardayo (@millardayo) September 8, 2016
'Usafirishaji wa mizigo kwa njia ya meli imeshuka duniani kote, jitihada za serikali zinafanyika ktk kujiimarisha' #Waziri_mkuu_Majaliwa
— millardayo (@millardayo) September 8, 2016
'Ni kweli tulikuwa na tatizo la sukari, tulitambua mapungufu na kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuagiza toka nje' #Waziri_mkuu_Majaliwa
— millardayo (@millardayo) September 8, 2016
'Kabla ya mwisho wa wiki hii tutatoa taarifa ya hali ya chakula kwa nchi nzima ikiwa ni pamoja na suala la sukari' #Waziri_mkuu_Majaliwa
— millardayo (@millardayo) September 8, 2016
'Kumekuwa na matukio ya mauaji ya raia na askari , hakika serikali itawakamata watuhumiwa wote na kuwachukulia hatua '#Waziri_mkuu_Majaliwa
— millardayo (@millardayo) September 8, 2016
ULIMIS MAJIBU YA WAZIRI NCHEMBA KWA MBOWE KUHUSU MADAI YA DENI LA TAIFA