Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo September 8 2016 limetangaza rasmi kukataa rufaa za vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid vya Hispania, FIFA wamekataa rufaa ya Real na Atletico iliyokuwa inafungia kufanya usajili katika madirisha mawili.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Real Madrid na Atletico walifungiwa na kamati ya nidhamu ya FIFA mwezi January kutofanya usajili kwa madirisha mawili kutokana na kukiuka kanuni za FIFA za usajili, kwa kufanya usajili wa wachezaji wa chini ya miaka 18 wasio raia wa Hispania.
Adhabu hiyo wataanza kuitumikia kuanzia sasa kwani awali ilishindika kutokana na vilabu hivyo kukata rufaa, hivyo Real Madrid na Atletico Madrid hawatoruhusiwa kufanya usajili hadi January 2018, adhabu hiyo pia inaambatana na faini ambapo Real Madrid watatakiwa kulipa pound 249,00 na Atletico pound 622,000, vilabu hivyo vinaweza kufanya usajili lakini havitaruhusiwa kuwatumia wachezaji hadi 2018.
GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1