Usiku wa Septemba 13 2016 ndio siku ambayo mashabiki wa soka ulimwenguni watashuhudia michuano ya klabu Bingwa Ulaya msimu wa 2016/2017 ikifunguliwa rasmi kwa michezo kupigwa barani Ulaya, moja kati ya michezo mikubwa siku ya leo ni mchezo kati ya Paris Saint Germain ya Ufaransa dhidi ya Arsenal ya England.
Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee rekodi 5 kuhusu mchezo wa Paris Saint Germain vs Arsenal
1- Stori kutoka mtandao wa 11vs11.com unaosha Arsenal na Paris Saitn Germain zilikutana March 29 1994 Paris na kutoka sare ya 1-1, lakini mchezo wa marudiano April 12 1994 Arsenal ilishinda kwa goli 1-0.
2- Katika mechi tano zilizopita kwa upande wa PSG kafanikiwa kushinda mechi tatu, kapoteza mchezo mmoja dhidi ya Monaco kwa kufungwa goli 3-1 hiyo ni baada ya mchezo wa Septemba 9 kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Saint Etienne.
3- Paris Saint Germain wameshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tisa ikiwa hii ni mara ya tano mfululizo kushiriki, lakini kwa upande wa timu za Ufaransa, Olympique Lyon ndio wanaongoza wameshiriki Ligi ya Mabingwa mara 14.
4- Toka Septemba 12 2012 Arsenal amecheza na vilabu vya Ufaransa jumla ya mechi 6, amefanikiwa kuibuka na ushindi michezo mitano na kapoteza mchezo mmoja pekee February 25 2015 dhidi ya Monaco kwa kufungwa goli 3-1 katika uwanja wake wa nyumbani.
5- Kwa ujumla Arsenal kacheza na vilabu vya Ufaransa mara 18 akiwa kashinda jumla ya michezo 11, sare michezo minne na kupoteza michezo mitatu.
Mechi za UEFA Champions League zitakazochezwa leo Septemba 13 2016. pic.twitter.com/EVLrWiEJ0U
— millard ayo (@millardayo) September 13, 2016
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0