Tukio la tetemeko la ardhi lililotokea September 10 2016 mkoani Bukoba na kusababisha vifo vya watu 17 limeendelea kuchukua nafasi katika vyombo mbalimbali vya habari na taasisi nyingine zikiwemo za Umma ambapo leo limefikishwa bungeni na kuruhusu baadhi ya wabunge kulijadili.
Kati ya wabunge waliopata nafasi ya kusimama bungeni na kuwasha kipaza sauti kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo ni pamoja na mbunge wa Muleba Professa Anna Tibaijuka ambaye baada kupata taarifa ya tukio hilo alifunga safari hadi Kagera.
Akichangia hoja ya ya wabunge kutoa mchango kwa wahanga wa tetemeko hilo alieleza bunge kwamba lisiingize siasa bali kila mmoja asimame kuchangia kwa ajili ya waathirika ambapo wabunge wote waliridhai kukatwa posho ya siku moja ili ikachangie kwenye kuwasaidia wahanga.
Video yake nimekuwekea hapa chini….
ULIMIS HII YA SHUHUDA ALIYESHUHUDIA MAMA MMOJA ALIVYOFARIKI KWENYE TETEMEKO BUKOBA