Septemba 12 2016 majina ya wanasoka mahiri waliyowahi kuvichezea vilabu vya Simba na Yanga Mohamed Banka na golikipa Juma Kaseja wameitwa na kocha John Mwansasu kuongeza nguvu katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni.
AyoTV ilimtafuta Mohamed Banka ambaye msimu huu hana timu ya Ligi Kuu, amelipokeaje kuongezwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni, vipi kuhusu kustaafu soka anafikiria? kuna changamoto yoyote ya soka la ufukweni na kawaida?
“Mimi nimepokea vizuri kwa mimi na Kaseja kuongezwa katika timu ya taifa ya beach soka, unajua mpira huu wa beach soka ni tofauti na kawaida hata sheria zake, kuhusu kustaafu kucheza soka bado sijapanga na unajua mpira kama ukitaka unaweza kucheza hadi ukiwa na miaka 38 hadi 40, kiukweli beach soccer kuna challenge”
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0