Baada ya klabu ya Manchester United inayofundishwa na kocha raia wa Ureno kufungwa mechi zake tatu mfululizo, usiku wa Septemba 21 2016 Man United walishuka tena dimbani kucheza mchezo wao wa EFL dhidi ya Northampton.
Katika mchezo huo ambao mashabiki wa Man United walikuwa na presha kubwa kama ambavyo Jose Mourinho alikasirishwa na kuwanyima mapumziko wachezaji wake, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1 wakiwa ugenini.
Man United ndio walianza kupata goli dakika ya 17 kupitia kwa Michael Carrick lakini lilisawazishwa dakika ya 42 na Alex Revell, kipindi cha pili Man United walikuja na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa kitu ambacho kilifanya wapate goli la pili dakika ya 68 kupitia kwa Ander Herrera na Marcus Rashford akahitimisha kwa kufunga goli la tatu dakika ya 75.
Matokeo ya mechi za EFL zilizochezwa Septemba 21 2016
-
Fulham 1 – 2 Bristol City
-
Queens Park Rangers 1 – 2 Sunderland
-
Southampton 2 – 0 Crystal Palace
-
Swansea City 1 – 2 Manchester City
-
West Ham United 1 – 0 Accrington Stanley
-
Stoke City 1 – 2 Hull City
-
Tottenham Hotspur 5 – 0 Gillingham
Magoli ya mechi ya Northampton vs Man United
https://youtu.be/-ycfizVC5nQ
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0