Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya taarifa ambayo ipo kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii kutoka gazeti la Mtanzania lenye kichwa cha habari, ‘Kinyongo kinasababisha kansa’
#MTANZANIA Utafiti uliofanywa nchini Marekani umebaini 61% ya magonjwa ya saratani yanasababishwa na tabia ya watu kushindwa kusamehe pic.twitter.com/z9jfbdWG9e
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
Utafiti uliofanywa nchini Marekani umebaini kuwa asilimia 61 ya magonjwa ya saratani yanasababishwa na tabia za watu kushindwa kusamehe wenzao waliowakosea.
Daktari Michael Barry ndio aliofanya utafiti huo nchini humo, ambapo sasa ameanzisha kliniki ya matibabu ya kusamehe Forgiveness Therapy.
Anasema watu wengi hushindwa kuwasamehe wenzao, hali ambayo huwasababishia msongo wa mawazo. ”wanakua hawana amani moyoni, muda mrefu wanakua na msongo wa mawazo dhidi ya wale waliowakosea, mwisho hujikuta wakiugua maradhi haya ya saratani.
Daktari bingwa wa kutibu magonjwa ya akili na mihemko, Steven Standiford wa Marekani anasema suala hilo lina ukweli ndani yake. ”wengi hushindwa kuhimili hali ya kutosamehe lakini pasipo kujua kwamba hali hiyo kujiua mwenyewe , kwani huwasababishia kupatwa kwa maradhi mbalimbali.
Akizungumza na Mtanzania Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage alisema anakubaliana na utafiti huo kwa kiasi fulani.
Katika utafiti wake , daktari huyo wa Marekani, Barry anaamini kupitia msamaha lolote linawezekana. Katika kitabu chake kipya kiitwacho ‘The Forgiveness Project’ (Mpango wa kusamehe) kinachoendelezea uvumbuzi wa ajabu wa jinsi ya kupambana na ugonjwa wa saratani, kuwa na afya njema na kuwa na amani. Dk. Barry anaelezea uchunguzi alioufanya juu ya umuhimu wa msamaha katika afya na unavyoweza kuleta tiba ya ugonjwa mkubwa kama saratani.
Source: MTANZANIA
Unaweza kupitia hapa habari nyingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania leo September 24 2106
#NIPASHE Vigogo 50 wapunguziwa viwango vya mishahara ili kukidhi agizo la Rais la kutaka kiwango cha juu kwao kiwe mil 15 na siyo mil 36-40 pic.twitter.com/jCipiJ04Lp
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#NIPASHE Mauaji ya wazee yaongezeka mwaka hadi mwaka na kwamba kwa sasa wastani wa wazee 500 wamekuwa wakiuawa kila mwaka pic.twitter.com/VmS6Ekxv8w
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#NIPASHE Hofu imetanda kwa wafanyakazi ATCL kutokana na baadhi yao kuwa ktk wasiwasi juu ya hatima ya ajira zao pic.twitter.com/XONyiz05RJ
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MWANANCHI Utata umeendelea kuhusu alipo muuaji aliyetajwa kesi ya kina Zombe, Koplo Saad Alawi pic.twitter.com/BFgXla9v4j
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MWANANCHI Waziri Mbarawa ameipa siku 90 Bodi ya ATCL kuhakikisha inaboresha hali ya utendaji pic.twitter.com/kl30j3r7CF
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MWANANCHI Siku tatu baada ya ajali za barabarani kusababisha vifo, Serikali yafuatilia kwa ukaribu mabasi yanayosafirisha abiria mikoani pic.twitter.com/zRMN0EqIWQ
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#JamboLEO Waliokamatwa kwenye nyumba iliyofanyikia mapambano ya polisi na majambazi Vikindu, Mkuranga waachiwa na kurejea kwenye nyumba hiyo pic.twitter.com/CfesdddWDK
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#JamboLEO Shirika la Speak Up for Africa limemtunukia Rais mstaafu Kikwete tuzo ya uongozi wa kisiasa na utetezi kwa makundi ya kijamii pic.twitter.com/JoSwgz2FS9
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#JamboLEO CHADEMA, CUF watoa kauli za kubeza hatua ya jeshi la polisi kuruhusu mikutano ya ndani pic.twitter.com/RP8nXSBi4c
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#JamboLEO NHIF yasema mabadiliko ya bei hayataathiri ubora wa huduma wala uwezo wa mwanachama kuhudhuria vituo vya matibabu pic.twitter.com/HjzPIuZgQx
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MAJIRA Viongozi wa dini wasema wameomba kuonana na Rais Magufuli kutokana na maono yao, wapinga uzushi unaoenezwa kuwa Rais amewakatalia pic.twitter.com/S0bfv7ABYe
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MAJIRA Muhimbili yatenga bil 3.4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba, ukarabati majengo, ununuzi wa vifaa ktk jengo la upasuaji na jengo la ICU pic.twitter.com/EMrkEi39bn
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MWANANCHI Utafiti wa mwanasayansi wa Kenya, Prof. Thumbi Ndung'u watoa matumaini ya kupatikana kwa tiba ya ugonjwa wa UKIMWI pic.twitter.com/lyqn9wsICb
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#TanzaniaDAIMA Muhimbili yapeleka madaktari 30 India kujifunza kwa vitendo jinsi ya kupandikiza figo na upasuaji wa kuweka kifaa cha usikivu pic.twitter.com/HMZPHEH9gA
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MWANASPOTI Majimaji yanasa udhamini mpya wa kampuni ya GSM na kuwa matajiri ghafla, GSM wamewarudishia kocha wao wa zamani Kally Ongalla pic.twitter.com/9sJ2pJJKjH
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#CHAMPIONI Wakati mkataba wa kiungo wa Simba, Mkude unaisha December mwaka huu, mwenyewe awambia Yanga kama wana nia waweke mezani mil 80 pic.twitter.com/0xxAbz7jMc
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV SEPTEMBER 24 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI