Mtu wangu nakusogezea taarifa hii kutoka visiwani Haiti. Wiki hii kuliripotiwa kutokea kwa kimbunga kikali kiliambatana na mvua pamoja upepo mkali ambao umevikumbuka visiwa hivyo. Kimbunga kilichopewa jina la Hurricane Matthew kimesababisha madhara makubwa kwa kuharibu miundo mbinu, majumba ya kuishi, watu wamepoteza maisha na wengine makazi ya kuishi.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti, Marc Vincent amesema kimbunga Matthew ni kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika miongo ya karibuni na bila shaka madhara yake yatakuwa makubwa.
Kimbunga Mathew ambacho ndicho kubwa zaidi katika visiwa vya Carebean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada ya kupitia Haiti na Cuba.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na serikali ya Haiti na wadau wengine kusambaza vifaa vya usaidizi kwa waathirika wa kimbunga Matthew kilichopiga Haiti hii leo. UNICEF inasema misaada hiyo ni pamoja na vidonge vya kutakasisha maji na vya kujisafi, wakati huu ambapo watoto zaidi ya Milioni Nne wanatarajiwa kuwa wameathiriwa na zahma hiyo.