Mwalimu wa shule ya msingi ungalimited Arusha, Batuli Hamadi Kisaya amekutana na millardayo.com na Ayo TV na amesimulia mkasa wa kutekwa uliomkuta. Mwalimu huyo anadai kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.
Mwalimu Batuli anasema October 3 mwaka huu wakati akitoka dukani alikutana na kijana mmoja na aliamriwa kupanda gari walilokuwa nalo, alipokuwa kwenye gari hilo mmoja wao akamwambia …‘wewe Batuli ulipoenda kumshtaki mkurugenzi wako uache mara moja na hapo ulipoenda kulalamika usirudi tena kama unapenda kazi yako, kama unapenda maisha yako tulia ufundishe na ufunge mdomo unyamaze kimya’
Baaada ya umbali kidogo Batuli anasema alianza kupiga kelele lakini akawa amezibwa puani na mdomoni akawa amepoteza fahamu na hakujua kilichoendelea na alipokuja kushtuka alijikuta Hospitali.
Batuli ameieleza Ayo TV na millardayo.com kuwa awali kabla ya tukio hilo la yeye kutekwa alipata barua ya kupanda cheo kuwa mratibu wa Elimu Kata ya Ngarenaro lakini baada ya wiki nne alipata barua ya kutenguliwa kutoka ofisi ya mkurugenzi. Hata hivyo alihoji kwa mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro kuhusu kutenguliwa kwake bila kuambiwa alichokosea.
Kusikiliza Full Stori Bonyeza Play hapa chini
ULIKOSA HII YA JAMAA BAADA KUTOA SIKU 30 KWA WEZI, AJIANDAA KUVUNJA CHUNGU? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI