Mtu wangu leo niko na Good news kutoka Equity Bank ambao wamefungua tawi jipya kabisa kule Zanzibar na hili likiwa ni tawi la 14 nchini Tanzania kama ishara ya kujikita zaidi katika uchumi wa utalii na fursa za uwekezaji Zanzibar.
Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Joseph Iha imebainisha kuwa wamezindua rasmi tawi hilo kama sehemu ya mpango wa mikakati ya benki ya kutanua wigo wa huduma bora kwa ajili ya ustawi wa jamii na kujenga uchumi wa watu wa Afrika.
>>>Tangu mwaka 2012 tulipoingia nchini Tanzania, tumefanya uwekezaji mkubwa ambao unaonesha mchango wetu katika ukuzaji wa uchumi wa Tanzania, Kufika kwetu Zanzibar kunaashiria dhamira yetu ya kusogeza huduma zetu bora:- Mkurugenzi Equity.
Benki yetu ina nia ya kupanua huduma zake barani Afrika na tunaendelea kujiweka katika nafasi muhimu za agenda zakifedha na kupitia hoja hii Equity Bank tunajiamini kwa kiasi kikubwa kuchangia katika mafanikio ya kiuchumi kwa hatua ya mwaka 2020:- Mkurugenzi Equity
Kitu kingine kizuri kutoka Equity Bank Tanzania, ni benki pekee nchini inayotoa mafunzo ya kifedha kwa lengo la kuwawezesha wateja kupata ujuzi wa elimu ya usimamizi wa fedha, hatua ambayo imekuza watu wa mkopo wa Fanikisha unao walenga wanawake.
Ikumbukwe kuwa Equity Bank Tanzania Limited ilianza shughuli zake mwaka 2012 na matawi mawili na kwasasa, benki hii ina jumla ya matawi 14 yanayofanya kazi ambayo ni Quality Centre, Arusha, Kariakoo, Golden Jubilee, Mwanza, Supreme Centre, Mwenge, Mbagala, Dodoma, Temeke, Diaspora Branch, Moshi, Mbeya na Zanzibar.
Equity Bank pia wanashirikiana na mawakala zaidi ya 800 nchini na ATM 17, pia Equity Bank Tanzania ni sehemu ya Equity Group Holdings ambayo ina benki na matawi katika nchi za Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Congo.
Unaweza kupata taarifa kupitia ukurasa wa Facebook Equity Bank Tanzania au tembelea www.tz.equitybankgroup.com.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV OCTOBER 13 2016? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI