Shirika la ndege la Kenya Airways limeahirisha safari zake tano za kwenda ndani na nje ya nchi leo October 16 2016 kutokana na upungufu wa Wahudumu wa ndege kazini.
Taarifa inasema sababu hasa ya kuahirisha safari hizo tano za Mombasa, Kilimanjaro, Juba, Maputo, Harare na Lusaka ni kutofika kazini kwa Wahudumu wa ndege ambao wamepangiwa zamu kwa wakati huo.
Imeelezwa kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo hawajaripoti kazini toka Ijumaa iliyopita ambapo shirika linaendelea kufatilia kujua chanzo ni nini na jinsi ya kutatua tatizo na Mwajiri.
Kwa utaratibu ndege za abiria huwa na masharti yake kwenye kila safari ikiwa ni pamoja na kuwa na namba flani ya idadi ya Wahudumu ndani ya ndege ambayo ni lazima itimie, sasa kutokana na Wahudumu wa Kenya Airways kuwa wachache imebidi ndege nyingine zisisafiri.
ULIIKOSA HII? UNAAMBIWA NDEGE MPYA ZA AIR TANZANIA UKIAHIRISHA SAFARI HUTOZWI PESA..
ULIYAKOSA MANENO YA MLINZI WA CHRIS BROWN KENYA? KAYAONGEA HAYA…..