Baada ya kutokea mgomo wa wafanyakazi siku ya Jumapili October 16, 2016 hatimaye Shirika la ndege la Kenya limefanikiwa kurudisha safari zake masaa kadhaa baada ya wafanyakazi wake kutofika uwanjani hapo jana kutokana na kilichodaiwa kushindwa kufikia muafaka wa madai yao na muajiri wao.
Ripoti iliyotolewa na shirika la ndege la Kenya imesema safari 67 zimefanyika tangu jana Jumapili saa kumi jioni, na ndege zote zilizofuata ziliondoka kwa wakati. Mgomo huo uliofanywa na wafanyakazi na watoa huduma ulianza ijumaa baada ya kutofautiana na uongozi wa shirika hilo.
Kutokana na mgomo huo safari za kwenda Maputo, Harare, Juba, Kilimanjaro na Mombasa zilifutwa.
Kurudishwa kwa huduma hizo kumekuja wakati marubani wa shirika hilo wametishia kugoma wakitaka maofisa wakuu wa shirika hilo kuondolewa. Inaelezwa kuwa hatma ya mgomo huo imebadilika baada ya mahakama ya migogoro kati ya wafanyakazi na waajiri kuingilia kati.
ULIMISS TAARIFA YA AFISA UHUSIANO WA ATCL KUHUSU UTARATIBU WA NDEGE MPYA ZA AIR TANZANIA? ITAZAME HAPA