Kwa muda mrefu tumekuwa na kampeni nyingi za kuhamasishana kuhusu upandaji miti au utunzaji misitu na wapo baadhi ya watu wetu ambao walishawahi kufikiwa na zawadi kuhusiana na issue ya Mazingira kwenye list yako ya watu waliopata zawadi kutokana na mazingira inabidi uwaongeze wananchi wa Kijiji cha Katurukila Morogoro.
Nimeipata ya Waziri wa Mazingira na Muungano ofisi ya Makamu wa Rais,January Makamba ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa kijiji cha Katurukila wilaya ya Kilombero Morogoro, kama kutambua mchango wao mkubwa katika utunzaji wa mazingira hasa eneo la Msitu wa Magombera.
Miongoni mwa maeneo ya Kilombero ambayo January Makamba ameyatembelea ni pamoja, Kilosa kwenye Mto Mkondoa, Kilombero, Msitu wa Magombera,Kijiji cha Kiturukila na Mto Lumemo Ifakara, kuhusu mgogoro wa msitu wa Magombera kati ya wanakijiji na mwekezaji Ramadhan Rashid Kuhuka, Waziri Makamba amesema kuwa tayari kesi imeshafika mahakamani na ni busara kuiachia mahakama.
Waziri Makamba pia ameagiaza taasisi ya kuapmbana na kuzuia rushwa TAKUKURU kuchunguza mazingira ya tuhuma za rushwa zilizoainishwa na wanakijiji juu viongozi wa kijiji na mwekezaji anayelalamikiwa, Waziri Makamba yuko kwenye ziara ya mazingira kwenye mikoa 10 ambayo ni Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora na Dodoma.
ULIKOSA HII YA JPM KUSEMA ALITAJWA MKE MMOJA MIMI NAFAHAMU WAKO WANNE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI