September 1 2016 shirika la nyumba la taifa NHC lilivamia na kuondoa vifaa katika chumba cha habari cha gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Mbowe Hotels chini ya Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Kampuni ya udalali ikishirikiana na NHC ilitoa vifaa hivyo nje huku Wafanyakazi wa ofisi hiyo wakiwa kwenye hali ya kushangazwa ambapo meneja wa kitengo cha kukusanya madeni NHC alisema taratibu zote zilifuatwa na Mbowe Hotels walishapewa notice sababu Mbowe anadaiwa.
Mbowe alifungua kesi mahakama kuu kitengo cha ardhi kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd akipinga uamuzi wa NHC kumuondoa katika jengo, leo October 18 2016 mahakama hiyo imefutilia mbali maombi hayo.
Katika uamuzi huo uliotolewa na mahakama hiyo na Jaji Sivangila Mwengesi amesema kuwa maombi yake hayana msingi na hivyo jaji Mwangesi amekubaliana na hoja za NHC na kusema kuwa aliondolewa katika jengo kisheria.
#MillardAyoUPDATES Mahakama kuu kitengo cha ardhi imefutilia mbali maombi ya Mbowe Hotel LTD kurudishwa ktk jengo la NHC. pic.twitter.com/0TvOJmtPlt
— millardayo (@millardayo) October 18, 2016
Baada ya Mahakama kuu kufutilia mbali maombi ya Mbowe Hotel LTD kurudishwa ktk jengo la NHC, mawakili wake wamesema watakwenda ngazi za juu pic.twitter.com/uLSKlfTawJ
— millardayo (@millardayo) October 18, 2016
ULIKOSA HII YA NHC WALOVYOTOA MALI ZA MALI FREEMAN MBOWE NJE KISA DENI LA BILIONI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINA