October 18 2016 Jeshi la Polisi Dodoma limetoa taarifa kwa vyombo vya habari Kuhusu hatua ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 13 kwa kosa la mauaji ya watafiti wa udongo watatu kutoka katika kituo cha utafiti Selian Arusha waliouawa kwa kukatwakatwa kisha kuchomwa moto.
Kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa amesema…>>>’Tumewafikisha mahakamani october 17 2016 watuhumiwa 13 kwa kosa la mauaji ya watafiti watatu yaliyotokea hivi karibuni mkoani hapa‘
‘Watu hawa waliuawa kwa kushambuliwa na kukatwa kwa silaha zenye ncha kali katika sehemu za miili yao kisha kuchomwa moto, kabla ya mauaji hayo, watuhumiwa walieneza taarifa za uongo kuwatuhumu watafiti hao kuwa ni wanyonya damu bila kuwahoji‘- Lazaro Mambosasa
‘Watafiti hao walikuwa wakifanya kazi kihalali tena wakiwa na vitambulisho kutoka halmashauri ya Chamwino na gari la serikali, watuhumiwa wengine walitoroka kwenda mafichoni, msako mkali unaendelea kuwasaka wote kisha kuwapeleka mahakamani kuungana na wenzao‘ – Lazaro Mambosasa
ULIMISS HII SERIKALI IMETENGA MABILIONI KUMALIZA UKOSEFU WA DAWA NCHINI