Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
#NIPASHE Scorpion aachiwa na kisha kusomewa upya mashitaka, ni uamuzi wa DPP aliyeomba baada ya hati ya awali kuwa na upungufu wa kisheria pic.twitter.com/zE7gphVDY5
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#NIPASHE Lema amesema chanzo cha ugomvi wao na RC Gambo ni 'kiongozi huyo wa serikali kupenda kuingilia majukumu ya wenzake bila sababu' pic.twitter.com/0lArUuAH8P
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#NIPASHE Walimu wakimbia vituo vya kazi kutokana na uhakiki wa vyeti unaoendeshwa na serikali, kubaini watumishi hewa na wasiokuwa na sifa pic.twitter.com/neRypnsoML
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#NIPASHE Wakati serikali ikisema imetoa zaidi ya bil 80 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu nchini, ni robo tu ya walioomba ndio watakaopata pic.twitter.com/Dg40XwOiny
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#NIPASHE Bodi ya wadhamini CUF jana ilifungua rasmi kesi mahakamani dhidi ya msajili wa vyama vya siasa, jaji Mutungi na Prof. Lipumba pic.twitter.com/Fwtqf8FkyO
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#NIPASHE Serikali imeongeza muda wa usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa kwa wiki mbili zaidi hadi kufikia October 31 pic.twitter.com/jQXCXUPxpb
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#NIPASHE Bosi Arusha adaiwa kumchoma moto kwa kumwagia petroli mpishi wa kampuni yake kwa madai ya kuchelewa kubandika maharage pic.twitter.com/4qEQp0BE7L
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MWANANCHI Imebainika wanafunzi 88,000 walioomba mikopo vyuo vikuu wengi hawatapata, uwezo wa HESLB ni kutoa mikopo kwa wanafunzi 21,500 pic.twitter.com/FVgbh2J9XI
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MWANANCHI Kuanzia mwakani ili mwanafunzi apewe cheti cha elimu ya msingi anatakiwa kukabidhi mti alioupanda siku ya kwanza alipoanza masomo pic.twitter.com/7waaYJMRWA
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MWANANCHI BoT yapeleka mahakamani ombi la kutaka hukumu ya Wafanyakazi 31 waliotimuliwa BoT 1993 kupitiwa upya pic.twitter.com/LKrNIdL5T7
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MWANANCHI Wilaya ya Moshi, K'njaro inaongoza kwa matukio ya udhalilishaji ukiwamo ubakaji na ulawiti, hususan kwa watoto wadogo pic.twitter.com/Vl50OYW2t7
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MWANANCHI Chuo cha The Golden Training Institute DSM chafungiwa na NACTE kutokana na kudahili wasiokuwa na sifa, wanafunzi 200 wahaha pic.twitter.com/rZ2bmnc2Jc
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MWANANCHI Hofu ya kugundulika kuwa na maambukizi ya VVU imewafanya watu wengi kutojitokeza kuchangia damu wilayani Igunga Tabora pic.twitter.com/BnykMtJVMq
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Jukwaa la wahariri, wadau wa habari waiomba kamati kutoa miez mitatu kuujadili kwa kina muswada wa sheria ya habari wa mwaka 2016 pic.twitter.com/eTfx5bgcE2
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa kuwa soda na chumvi vinaongoza kwa kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwamo shinikizo la damu pic.twitter.com/cDxdyOeImo
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Gambo, Lema wamuibua Dk, Slaa, kupitia mitandao wa kijamii Dk. Slaa amemshambulia RC Gambo huku akimtaka aache siasa za majitaka pic.twitter.com/o3qkIaLnEi
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Halmashauri ya jiji la Mwanza inapoteza bil 1.3 kila mwaka za pango ktk majengo 1,024 inayoyamiliki kutokana na mikataba ya ovyo pic.twitter.com/gOjrBWG9wl
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Utafiti mpya uliofanyika mataifa 42 ulaya wapinga nyama, maziwa kusababisha maradhi ya moyo watupia lawama viazi mviringo, nafaka pic.twitter.com/TqTCsDCf7o
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Jumla ya bil 20 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya utengenezaji wa meli tatu za kisasa katika Ziwa Nyasa. pic.twitter.com/lgaoBCPChf
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Mkuu wa shule ambayo mwanafunzi anayehusishwa na 'panya road' anasoma, amesema tabia yake shuleni haiendani na inayodaiwa mtaani pic.twitter.com/CFGvJFQDA6
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa kuwa tunda la pera lina faida nyingi ikiwamo kusaidia kurutubisha mayai ya uzazi kwa kuwa yana madini yaitwayo Folate pic.twitter.com/jCXSkG5J9E
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#TanzaniaDAIMA BAVICHA yampa siku saba Waziri Ndalichako kueleza hatima ya wanavyuo waliokosa mikopo ya elimu ya juu pic.twitter.com/ilF27Shnrf
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#UHURU Wanafunzi vyuo vikuu waruhusiwa kulipa nusu ada ndipo waweze kusajiliwa huku wakisubiri taarifa ya uhakiki ya bodi ya mikopo pic.twitter.com/NrswDLTtDQ
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#BINGWA Klabu ya Fanja FC ya Oman imeipatia mil 22 Simba kama malipo ya usajili wa straika wa zamani, Danny Lyanga aliyejiunga Fanja FC pic.twitter.com/J4QLh4kBvh
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#BINGWA Kocha wa zamani wa Azam FC, Stewart Hall apewa mkataba wa miaka miwili ktk klabu ya AFC Leopard inayoshiriki ligi kuu ya Kenya pic.twitter.com/aMxBZt6p2s
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
#BINGWA Baada ya klabu ya Chippa United ya A.kusini kuvutiwa na Kichuya, yeye asema yupo tayari kuondoka Simba iwapo klabu hiyo itamhitaji pic.twitter.com/zDELY2SSCU
— millardayo (@millardayo) October 20, 2016
ULIKOSA TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI KUHUSU SHAMBULIO LILOUWA MAJAMBAZI SITA DSM? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI