Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
Moja ya habari kubwa iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii kutoka gazeti la Tanzania Daima yenye kichwa cha habari ‘Mkurugenzi ampigisha deki mwalimu’
#TanzaniaDAIMA Mkurugenzi Misungwi, Mwaiteleke adaiwa kumuamuru mwalimu kudeki darasa mbele ya wanafunzi baada ya kukuta madarasa ni machafu pic.twitter.com/otDN52kSy6
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
Habari kutoka gazeti la Tanzania Daimi imedai kuwa jana October 20 2016 mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliud Mwaiteleke ameingia kwenye kundi la wakurugenzi wanaowanyanyasa na kudhalilisha watumishi wa chini baada ya kudaiwa kumuamuru mwalimu wa shule ya sekondari ya Shilala, Hamis Sengo, kudeki darasa zima, mbele ya wanafunzi wake.
Inaelezwa kuwa mkurugenzi huyo alifika shuleni hapo akiwa na watendaji wengine wa wilaya na kukuta madarasa yakiwa machafu, ndipo aliamuru mwalimu huyo kudeki darasa zima mbele ya wanafunzi wake, jambo ambalo limepingwa vikali na kulaaniwa na chama cha walimu ‘CWT’ wilayani humo.
Unaweza kuzipitia hapa chini habari zingine zilizoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania leo October 21 2016
#NIPASHE Matumaini mapya waliokosa mikopo vyuoni, baada ya kamati ya bunge ya maendeleo ya jamii kuweka kwenye ratiba yake suala la mikopo pic.twitter.com/MIwONw8SNj
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#NIPASHE Waziri mkuu, Majaliwa amemwagiza mkurugenzi NSSF awaandikie barua waajiri wanaodaiwa na NSSF kuwataka wawasilishe fedha wanazodaiwa pic.twitter.com/yGxioTrwcI
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa kuwa kuna vilio kila kona sekta ya afya nchini kutokana na wanaofika hospitali mbalimbali kwa matibabu kukosa dawa pic.twitter.com/aCV7r6JnTI
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MTANZANIA Kichocho cha tumbo hushambulia viungo vya uzazi vya mgonjwa na kusababisha ugumba, saratani ya kizazi, maambukizi VVU kwa urahisi pic.twitter.com/m3fNa5Jq0T
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MTANZANIA Wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima walia njaa kutokana na kupunguziwa fedha za kujikimu pic.twitter.com/amJhhEuMBr
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Serikali yarejesha sh 8500 kwa wanafunzi vyuo vikuu ni baada ya malalamiko kutoka vyuo mbalimbali kuingiziwa fedha pungufu pic.twitter.com/YLhkkIJdC6
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Ofisi ya waziri mkuu imezitaka wizara, mikoa kuchukua hatua kukabiliana na tishio la njaa ikiwamo kuzuia nafaka kutengeneza pombe pic.twitter.com/CRG35gkq8F
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Kamati ya bunge ya viwanda yakataa ripoti ya wizara baada ya wajumbe kushindwa kutembelea miradi kutokana na ukosefu wa fedha pic.twitter.com/CWdYya5K5J
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Kaya feki 32,456 zapokea fedha TASAF kupitia mpango wa kusaidia kaya maskini, kati ya waliopokea fedha ni watu waliofariki 7,819 pic.twitter.com/lNa7KgShV1
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Ng'ombe 25 Rufiji wamekufa baada ya kudaiwa kula nyasi zenye sumu machungani kwenye kijiji cha Mbunjumvueni pic.twitter.com/rmvDbUTgxP
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Wajumbe halmashauri kuu CCM Mbozi Songwe wamewavua madaraka viongozi wawili waandamizi mmoja kwa kukigawa chama na mwingine ulevi pic.twitter.com/ZVEZ7KAZWO
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Utafiti Uingereza unaonesha utumiaji wa wastani wa Aspirini kila siku hupunguza uwezekano wa kupoteza maisha kutokana na kansa pic.twitter.com/BjtcAnreIa
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Wataalamu wanasema tatizo la mtindio wa ubongo kwa watoto linachangiwa na ukosefu wa oksijeni wakati wa kujifungua pic.twitter.com/NZzxyc8rdV
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Imeelezwa kusimama kwa saa tatu ni zoezi lenye faida kiafya sawa na mtu anayeshiriki kwenye mashindano ya kukimbia pic.twitter.com/I6dxBqkEwx
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Trump ajipanga kukataa matokeo, asema amegundua waliojiandikisha kwenye daftari la wapigakura, wengi siyo raia wa Marekani pic.twitter.com/F4kafSih8F
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#HabariLEO Waziri Mwijage amesema ataifumua na kuiunda upya TBS na ameshaanza kutafuta vijana 136 lengo ni kudhibiti bidhaa chini ya viwango pic.twitter.com/JVhJRjOU72
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#HabariLEO Ofisi ya DPP imesema itaendelea kutekeleza adhabu ya kifo kisheria ingawaje kibinadamu hakuna ambaye angependa kushuhudia hilo pic.twitter.com/b0Mpsyx7Rl
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#JamboLEO Kaya zaidi ya 450 hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao 150 kubomolewa Goba, DSM kwa madai ya kujengwa eneo lisilo lao pic.twitter.com/MMTAf0GD0f
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#TanzaniaDAIMA Mkurugenzi Misungwi, Mwaiteleke adaiwa kumuamuru mwalimu kudeki darasa mbele ya wanafunzi baada ya kukuta madarasa ni machafu pic.twitter.com/otDN52kSy6
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MAJIRA Utafiti uliofanywa China umebaini kuwa ukila chakula chenye viungo hasa pilipili utaishi maisha marefu zaidi duniani pic.twitter.com/0v1doKUMkX
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
#MWANANCHI Serikali imelipa bil 722.7 kati ya bil 964.2 za madeni ya michango, ambayo Serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini pic.twitter.com/N0bZ13k5in
— millardayo (@millardayo) October 21, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV, OCTOBER 21 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI