Kwenye vitu ambavyo inawezekana hukua ukifahamu au kufikiria kama kuna uwezekano wa kuwepo ni pamoja na hii issue ya upatikanaji wa mafuta aina ya Diesel kwenye visima vya maji Mkoani Songwe.
Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe January Makamba kwenye ziara yake ya mazingira amefanikiwa kufika katika mji wa Mloo ulioko kwenye mkoa wa Songwe na kupokea taarifa ya mazingira ya Mkoa ambayo imebainisha tatizo la uwepo wa mafuta ya Diesel kwenye visima vya maji na kuelezwa kuwa mafuta hayo siyo mafuta ghafi yanayotakiwa kupatikana ardhini.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa uvamizi wa shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji inatishia uhai wa vyanzo hivyo,Waziri Makamba ameahidi kusaidia upatikanaji wa wataalamu ili kuweza kutambua chanzo cha tatizo hilo la uwepo wa mafuta katika visima vya maji na kutambua njia sahihi za kukabiliana na tatizo hilo.
Vilevile Waziri Makamba amefika katika Wilaya ya Ileje ambapo pia amepokea taarifa ya Mazingira ya Wilaya na kupongeza juhudi kubwa za wilaya ya Ileje katika utunzaji wa mazingira hasa eneo kubwa la misitu uliopo katika lililopo katika Wilaya hiyona kuahidi pia kuzisaidia Halmashauri za Wilaya na Vijiji namna sahihi na bora zaidi ya kuandaa sheria ndogo za mazingira ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa Mazingira.
Umemiss kuyafahamu Mambo 7 ya kutikisa treni ya kisasa,Utata Mamilioni ya Lipumba na mengine?Bonyeza play hapo chini kutazama.