Waziri wa Mazingira na Muungano, Ofisi ya Makamu wa Rais January Makamba ameaendelea na ziara yake ya mazingira katika Mikoa 10 ambapo akizungumza na wananchi wa Kata ya Nankanga, Wilaya ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa eneo la Forodhani lililopo katika fukwe za Ziwa Rukwa ametanabaisha kuwa kina cha Ziwa hilo limepungua kwa takribani mita 3 katika kipindi cha miaka 16 ambapo mwaka 2000 kina hicho kilikuwa mita 6 na hivi sasa ni takribani mita 3 pekee.
Waziri Makamba amesema serikali itatangaza eneo la Ziwa Rukwa kuwa eneo nyeti la Mazingira na kuagiza kusitishwa kwa shughuli zote za Kilimo na Ufugaji zinazofanyika katika kingo za Ziwa Rukwa na kutoa siku 5 kuhakikisha agizo hilo limetekelezwa.
Aidha Waziri Makamba ameainisha kuwa Serikali itachukua hatua za muda mrefu kuokoa Ziwa hilo lakini katika hatua za awali za kuokoa Ziwa Rukwa ameagiza kuwa kuanzia october 28 mwaka huu haitoruhusiwa kufanya shughuli za Kilimo na ufugaji ndani ya Mita 60 za ukingo wa Ziwa kama inavyotakiwa na Sheria ya Mazingira, Sheria ya Maji na Sheria ndogo za Serikali za Mitaa.
ULIKOSA MANENO YA WAZIRI MWIJAGE KWA WANAOPENDA ELIMU ‘MSELELEKO’? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI