Ikiwa leo ni October 25, 2016, Rais John Pombe Magufuli anatimiza mwaka mmoja tangu alipopigiwa Kura na wananchi wa Tanzania na kumchagua kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jarida linalofanyia tafiti watu maarufu na shughuli wanazozifanya la Forbes, limetangaza watu wanaowania tuzo ya Mtu Maarufu wa Mwaka.
Forbes wamemtaja Rais Magufuli kama kiongozi ambaye amefanikiwa kuongeza kiwango cha uchumi wa nchi yake huku akishindana na watu wengine kama Michael Le Roux ambaye ni muanzilishi wa Capitec Bank nchini Afrika Kusini, Benki ambazo zimeonekana kuwa rahisi zaidi kutumika na wananchi wa Afrika Kusini.
Wengine ni Thuli Madonsela, Ameenah Gulib pamoja na watu wa Rwanda.
Anachuana na watu wengine wanne wakiwemo: Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda. Tuzo hii iliwahi kutolewa pia kwa mtanzania Mohamed Dewji mwaka 2015.
Mtu wangu unaruhusiwa kumpigia kura ya ushindi Rais Magufuli kupitia Hapa. Kumbuka mwisho wa kupiga Kura ni November 17, 2016 na tuzo hiyo itatolewa Nairobi Kenya.
ULIPITWA NA MAZOEZI YA JESHI LA POLISI YALIYOSHTUA WATU MITAANI? TAZAMA VIDEO HII