Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 umeendelea leo kwa Mabingwa watetezi klabu ya Dar es Salaam Young Africans kushuka dimba la Uhuru kucheza dhidi ya JKT Ruvu bila uwepo wa kocha wao mkuu muholanzi Hans van Pluijm aliyejiuzulu nafasi yake hiyo ndani ya Yanga.
Mchezo wa Yanga dhidi ya JKT Ruvu ndio mchezo wa kwanza kucheza baada ya kocha wao mkuu Hans van Pluijm kujiuzulu, wakati wengi wakiwa wanatafuta sababu za msingi za kwa nini uongozi wameruhusu ajiuzulu, timu yao leo imeaiadhibu JKT Ruvu wa goli 4-0.
Magoli ya ushindi wa Yanga yalifungwa na mzambia Obrey Chirwa dakika ya 6, Amissi Tambwe aliyefunga mawili dakika ya 64 na Simon Msuva akafunga goli la tatu dakika ya 83 kabla ya Tambwe kuhitimisha idadi ya magoli hayo kwa kufunga goli la mwisho dakika ya 92, Yanga mchezo ujao atacheza dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Uhuru.
Msimamo wa #VPL ulivyo kwa sasa baada ya mchezo wa Yanga 4-0 #JKTRuvu kumalizika. pic.twitter.com/W38LcEwnmC
— millard ayo (@millardayo) October 26, 2016
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0