Moja kati ya maeneo ya utalii ambayo Tanzania tumebahatika kuwa nayo ni pamoja na hii Mbuga ya Katavi ambayo utambulisho wake mkubwa ni nembo ya Viboko.
Lakini pia Viboko hao wengi wanaishi kwenye maisha magumu baada ya kuwepo kwa baadhi ya watu walioamua kuchepusha mto na kuharibu vyanzo vya maji, jambo ambalo limesababisha maji kutowafikia Viboko ambao maisha yao kwa asilimia kubwa yanategemea kuwepo kwa maji.
Na mmoja kati ya watu waliofika eneo hilo la Mto Katuma na kujionea ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi kutembelea maeneo mengi nchini ili kujionea hali ya mazingira ilivyo.
Nimezipata pia Picha za Mbuga ya Katavi ambayo inatajwa kuwa na Viboko wengi lakini mazingira wanayoishi yamekuwa hatari kwako kutokana na kukosekana kwa maji ya kutosha.
ILIPITWA NA KAULI YA WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI CHARLES MWIJAGE KUHUSU AGIZO LA RAIS MAGUFULI JUU YA SUKARI YA BAKHRESA