Ebwana headline za utafiti zimekuwa zikichukua nafasi sana hivi sasa ambapo kwenye mitandao ya kijamii moja ya stori iliyochukua nafasi ni pamoja na ile inayosema kwamba ‘Kulala na nguo za ndani chanzo cha ugumba‘ millardayo.com ikaona imtafute Dr. Kisaka Stephen ambaye ni daktari wa magonjwa ya binadamu.
‘Nimepitia majalada mbalimbali za afya na maswala ya uzazi lakini kitaalamu inaeleza kwamba kulala na nguo kwa mwanamke hakuna madhara yoyote kwakuwa viungo vyake vipo ndani lakini kwa mwanaume madhara yapo endapo kutakuwa na uzalishaji wa joto katika maeneo yake ya uzazi‘ –Dr. Kisaka Stephen
‘Yapo mambo mengi yanaweza kuchangia au kusababisha mwanamke kutopata ujauzito ikiwa ni pamoja na magonjwa ya njia ya uzazi, kuziba kwa njia za uzazi pamoja na magonjwa sugu aliyowahi kuyapata awali‘ –Dr. Kisaka Stephen
‘Kwahiyo tunasisitiza kwamba katika possition ya kutopatikana kwa mtoto tatizo linaweza kuwa kwa mama au kwa baba ingawa kwa asilimia kubwa tatizo huwa kwa wakinamama‘ –Dr. Kisaka Stephen
Unaweza kuendelea kumsikiliza Dr. Kisaka Stephen kwenye hii sauti hapa chini..
MAJIBU YA LINEX KUHUSU KUHAMIA KWENYE MUZIKI WA INJILI