Wakati fedha nyingi zikitajwa kutumika kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali wanaoenda kutibiwa nje ya nchi kutokana na huduma hizo kushindwa kupatikana hapa nchini.
Good news leo zimetolewa na Hospitali ya Muhimbili kupitia kwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma, Aminiel Bubwerwa Aligaesha ambaye amefafanua ulipofikia mpango wa kupunguza safari za kwenda nje kutibiwa wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli.
Aminiel Bubwerwa Aligaesha, amesema…..>>>’Ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017 Hospitali itaweza kupandikiza figo hapa hapa nchini na kupanua huduma za kusafisha figo kutoka uwezo wa kuwa na mashini 23 mpaka kufikia machine 50′;-Aminiel Aligaesha
>>>’Hospitali ya Taifa Muhimbili imepeleka nchini India wataalamu 18 wa fani mbalimbali kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upandikizaji figo kwa watu wenye matatizo ya figo na timu hiyo inatarajia kurejea mwishoni mwaka. Mgonjwa mmoja anayepandikizwa figo nje ya nchi pia hugharimu kiasi cha shilingi milioni 40 hadi 60′;-Aminiel Aligaesha
>>>’Hospitali ilipeleka watalaamu saba India katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi ili wakajifunze kwa njia ya vitendo jinsi ya kufanya upasuaji na upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto. Wataalamu hawa wamerudi. Gharama za kupandikiza kifaa cha usikivu kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi milioni 80 hadi 100 anapopelekwa nje ya nchi’-Aminiel Aligaesha
ULIKOSA KUTAZAMA ALICE TUPA WA AYO TV AKICHAMBUA MAGAZETI YA TANZANIA YA NOVEMBER 1 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI