November 9 2015 ikiwa ni siku nne baada Rais Magufuli kuapishwa alifanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kukutana na changamoto kadhaa ambapo alitoa maagizo kwa Uongozi wa Hospitali kwamba, mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) na Computerized Tomography Scan (CT-Scan) ambazo zilikuwa zimeharibika ziwe zinafanya kazi katika kipindi cha siku 14.
Maagizo mengine ni pamoja na wagonjwa waliolala chini wawe wamepata vitanda pamoja na wagonjwa wote kupata dawa kupitia maduka ya dawa yaliyopo Hospitalini hapa. Na kuagiza Bohari Kuu ya Dawa (Medical Stores Department–MSD), kufungua duka la dawa ndani ya Hospitali ili kuondoa ukosekanaji wa dawa ambao ulikuwa unasababisha wagonjwa walazimike kununua dawa katika maduka binafsi yaliyopo nje ya Hospitali.
Leo November 1 2016, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu Rais Magufuli atoe maagizo hayo, mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Bubwerwa Aligaesha wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli amebainisha utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli
>>>’Matengenezo ya mashine ya MRI yalifanyika kikamilifu na hadi hivi sasa mashine hii inaendelea kufanya kazi vizuri ambapo kwa kipindi cha December 2015 hadi October 25, 2016 wagonjwa 17,951 wamepimwa ukilinganisha na wagonjwa 1,911waliopima December 2014 hadi October 2015′;-Aminiel Bubwerwa Aligaesha
>>>’Mashini ya CT-Scan ilitengenezwa kikamilifu na hadi hivi sasa mashine hii inaendelea kufanya kazi vizuri ambapo kwa kipindi cha December 2015 hadi October 2016 wagonjwa 10,259 wamepimwa ukilinganisha na wagonjwa 3,319 waliopimwa December 2014 hadi October 2015′;- Aminiel Bubwerwa Aligaesha