Kama ni mpenzi wa soka najua jana utakuwa ulisikia zile headlines za Simba baada ya kucheza mechi 13 za Ligi Kuu bila kufungwa msimu huu wa 2016/2017 akiwa katoka sare mechi mbili na kushinda mechi 11, jana alipoteza kwa mara ya kwanza dhidi ya African Lyon kwa goli 1-0, goli likifungwa na Abdullah Msuhi dakika za nyongeza kabla ya mchezo kumalizika.
millardayo.com imempata Hassan Is-haka katika exclusive interview ambaye alikuwa Simba baadae akasimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kutuhimiwa kumjibu vibaya kocha Jackson Mayanja baadae akasamehewa ila akavuliwa unahodha mwisho wa msimu akatolewa kwa mkopo African Lyon.
“Hakuna kitu kizuri kama kuingia uwanjani na kutoka na point tatu, umeona tumecheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kujiamini hatukucheza faulo nyingi na tulikuwa tunaziba gape, hatukucheza mpira wa kupoteza muda sema kama beki wa kati lazima tupoze mashambulizi kitu ambacho kimesaidia kushinda”
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0