November 10 2016 wabunge wa Bunge la Afrika Kusini wamefuta kabisa pendekezo la kupiga kura ya kutokua na imani dhidi ya Rais wa Afrika Kusini wa nchi hiyo Jacob Zuma pamoja na kuwepo madai ya hivi karibuni kuhusu ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa kiongozi huyo.
Kwa mujibu wa Radio France International, Uchunguzi uliofanywa na tume ya kukabiliana na ufisadi nchini Afrika Kusini umesema kuwa jopo la majaji linatakiwa kuundwa ili kuchunguza madai ya uhalifu katika serikali za Rais Zuma.
Uchunguzi huo ulipata ushahidi kwamba familia tajiri ya mfanyabiashara Gupta yenye uhusiano mkubwa na Zuma huenda ilikuwa na ushawishi mkubwa katika uteuzi wa baraza la mawaziri wa Afrika Kusini.
Taarifa iliyotolewa baada ya uchunguzi wa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini humo wiki iliopita ilizua madai ya kutokuwepo kwa nidhamu ya madaraka dhidi ya Rais Jacob Zuma.
Baada ya kupigwa kura za kutoa mapendekezo ya kutokua na imani na Rais, Chama cha Rais Zuma ANC chenye wabunge wengi katika bunge na mswada huo wa upinzani kilishinda kwa kura 214 dhidi ya 126 za upinzani.
Hii ni imekua ni mara ya tatu kwa Rais Zuma kupigiwa kura na wabunge kutokuwa na imani naye kulikofanywa bungeni katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja.
VIDEO: Rais Magufuli amefanya ziara ya kutembelea wagonjwa akiwemo mkewe Janeth aliyelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Bonyeza Play hapa.