Alfajiri ya kuamkia November 11 2016 ulichezwa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la dunia 2018 uliovutia hisia za mashabiki wengi, mchezo huo ulikuwa unazikutanisha Brazil vs Argentina katika uwanja wa Mineirao Brazil lakini ni mchezo ambao ulikuwa unawakutanisha nyota wa FC Barcelona Lionel Messi na Neymar.
Katika mchezo huo Argentina wameingia uwanjani wakiwa na hali mbaya katika msimamo ambapo kwenye nafasi waliyopo hawawezi kucheza Kombe la dunia na watahitaji kushinda michezo kadhaa ili kufufua matumaini ya kucheza Kombe la dunia 2018 baada ya kujikuta wakipigwa 3-0 na Brazil.
Kiama cha Argentina kilitolewa na Philip Coutinho dakika ya 29 baada ya kupokea assist safi ya Neymar ambaye baadae alifunga goli la pili dakika ya 45 kwa assist ya Gabriel Jesus, kabla ya Jose Paulinho kukomelea msumari wa mwisho dakika ya 58 uliomfanya Lionel Messi na wenzake watoke vichwa chini uwanjani.
Msimamo wa Kundi waliopo Brazil na Argentina, kwa kawaida wanne wa juu wanafuzu kucheza #WC2018 na watano anacheza Playoffs ili kufuzu. pic.twitter.com/QCaIbtrHp2
— millard ayo (@millardayo) November 11, 2016
VIDEO: Magoli yote ya Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0