Mamia ya wananchi pamoja na Viongozi wa Serikali, wameungana na familia katika mazishi ya aliyewahi kuwa Mbunge na waziri wa zamani, Joseph Mungai yaliyofanyika November 12 katika mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.
Mungai aliwahi kuwa mbunge wa Mufindi kupitia CCM na aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini katika awamu ya kwanza hadi ya nne akiwa waziri wa Elimu na Utamaduni, Waziri wa kilimo na Maendeleo, waziri mambo ya ndani, na alifariki dunia November 8 2016.
Nimekuwekea picha za viongozi mbalimbali wa kiserikali na wananchi walivyoshiriki mazishi katika jimbo alilowahi kuliongoza Mufindi mkoani Iringa.
VIDEO: Waziri Lukuvi anayo maneno mazito kuhusu marehemu Joseph Mungai. Unaweza kuitazama Video hii