Masaa machache baada ya kutokea Tetemeko lenye ukubwa wa Richa 7.8 katika eneo la Cheviot Kaskazini mwa Christchurch huko New Zealand na kuua watu wawili, imeripotiwa kutokea Tetemeko lingine nchini humo lenye ukubwa Richa 6.3 katika eneo la South Island.
Tetemeko hilo limetokea leo Jumatatu November 14, 2016 umbali wa maili 60 kutoka eneo Christchurch, baada ya tetemeko lingine lilikuwa na mgandamizo wa Tsunami kuipiga New Zealand usiku wa kuamika Jumatatu.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa New Zealand John Key amethibitisha kutokea kwa matetemeko hayo na vifo vilivyotokea, huku idara ya majanga nchini humo ikiwataka raia wake kuhamia maeneo ya juu ili kujikinga na madhara yatakayotokea na bado wanafanya uchunguzi kujua madhara ya kibinadamu na miundombinu yaliyotokea.
New Zealand inatajwa kuwa katika eneo lenye mgandamizo mkubwa miamba ambayo hukatika au kupasuka kutokana na kuwa karibu na bahari ya Pacific Ocean ambayo hukumbwa na vimbunga vya Tsunami.
New Zealand iliwahi kupigwa na tetemeko kubwa mwaka 2011 katika eneo la Christchurch na kuua watu 185.
Nimezipata picha 28 za madhara yaliyotokea baada ya matetemeko hayo kutokea nchini New Zealand leo Jumatatu.
VIDEO: Alice Tupa anazo stori zote kwenye Magazeti ya leo November 14, 2016, Tayari nimekuwekea hapa.