Usiku wa leo November 24 2016 timu ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa tano wa hatua ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya timu ya Rapid Wien ya Austria.
KRC Genk katika mchezo huo wa tano walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Luminus, Genk wakiwa nyumbani walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 55 dhidi ya wageni wao Rapid Wien, kitu ambacho kimewasaidia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 11.
Msimamo wa Kundi F linaloongozwa na KRC Genk inayochezewa na mtanzania @samatta77 pic.twitter.com/bTBkmYVnRz
— millard ayo (@millardayo) November 24, 2016
Kwa matokeo hayo Genk na Atletico Bilbao wanafuzu hatua inayofuata kutokana na wote kuwa na point 9 wakati Rapid Wien na Sassuolo ya Italia watakuwa wanasubiri mchezo wa mwisho wa kukamilisa ratiba, maana hata wakishinda watakuwa na point nane kila mmoja, point ambazo hazitoshi kuipiku Genk wala Atletico Bilbao.
Matokeo ya mechi 24 za Europa League zilizochezwa usiku wa November 24 2016. pic.twitter.com/w1vBXmrrzr
— millard ayo (@millardayo) November 24, 2016
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0