Siku chache baada ya Rais Magufuli kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, hatimaye Bodi za taasisi nyingine muhimu za Serikali zimeanza kuwajibika kwa kufanya maamuzi ya kubadili mifumo ya utendaji, na moja ya taasisi zilizofanya mabadiliko ni Shirika la Ndege Tanzania ATCL.
Leo November 25, 2016 Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege Tanzania ATCL chini ya Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Emmanuel Korosso, imetoa maagizo ya kuondolewa kwa wakurugenzi wa idara tano katika menejiment ya ATCL na huku ikimbakiza Mkurugenzi Mtendaji Ladslaus Matindi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji, wakurugenzi walioondolewa kwenye idara ni pamoja na Mkurugenzi wa Biashara, Mkurugenzi wa Ufundi, Mkurugenzi wa Oparesheni, Mkurugenzi wa Fedha na Mkurugenzi wa Usalama na kwa upande wa wafanyakazi wengine shirika linaendelea kuwafanyia mchujo.
Taarifa kamili ipo hapa. Bonyeza play kutazama.
AUDIO: Simu ya Rais Magufuli kwenda kwa RC Paul Makonda kuhusu maelezo ya Dar Mpya! Bonyeza play hapa chini