Kila siku asubuhi huwa nazisogeza Headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account zangu za Twitter, Facebook na Instagram kupitia jina la @millardayo.
#MWANANCHI Baada ya kumfanyia fujo jirani yake Mch. Anthony Lusekelo "Mzee wa Upako" ameibuka na kudai kuwa hashindani na watu walioshindwa pic.twitter.com/o8NUuTPKwB
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, mchungaji huyo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako ameibuka kanisani kwake na kusema msemo wake wa kawaida kuwa, ‘watashindana lakini hawatashinda.
Pia alisema kuwa alitaka kusema jambo, lakini hatazungumza kama wengi walivyodhani. Lusekelo aliyasema hayo jana jioni katika ibada ya Ijumaa kanisani kwake, Ubungo Kibangu ambako mwandishi wa Mwananchi alihudhuria.
“Nimeyaona magazeti hapa, ooh Mzee wa Upako, ooh Mzee wa Upako, sisemi. Sasa leo yupo hapa, na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke,” alisema huku akishangiliwa na waumini wake.
Kabla ya kuzungumza, Lusekelo aliingia kanisani akiimba wimbo wa kuabudu ‘Niguse Tena’ huku waumini wote wakiwa wamesimama.
Akiwa amevalia shati jeupe la kitenge na suruali nyeusi huku kanisa likiwa limezingirwa na walinzi kila kona, mchungaji huyo aliingia na kusimama madhabahuni kisha kuwasalimu waumini: “Nawasalimu katika jina la Bwana.”
Baada ya salamu hiyo, alianza kuimba wimbo mwingine na waumini hao wakaanza kuimba pamoja naye huku wakipita mmoja mmoja mbele kumtuza fedha.
Wimbo ulipoisha, waumini waliketi na Lusekelo alianza kuhubiri kwa kufungua Biblia katika kitabu cha 2 Timotheo 4.
Katikati ya mahubiri hayo, alidokeza na kusema kuna watu walikuwa wanasubiri kuona Mzee wa Upako hayupo na wanataka aseme, lakini hatasema chochote.
“Kuna kitu nilikuwa nataka nikiseme, lakini sitakisema ili waendelee kusema haohao waliokuwa wanasema. Sisemi chochote. Hao waliosema wakawaulize wenyewe,” alisema bila kufafanua zaidi.
Ingawa alisema hatasema chochote, mahubiri yake yalionekana kama kujibu mapigo.
“Imani yangu ndiyo ilikuwa mwisho, kwa sababu maadui watakuwa wengi lakini watajikuta wanapiga risasi kule, kumbe adui yupo huku… vita ni kutulia,” alisema.
“Adui yako hataacha kuwa adui yako. Jiepushe sana na watu hao. Lakini mimi ninaamini Mungu atawalipa sawa na amri yake wakati ukifika.” Aliendelea na kusema wanadamu wamekengeuka na kuziacha njia za uzima na kuzigeukia njia zao wenyewe.
“Wakati wote watu watakataa kusikia ule ukweli, Ogopa sana anayekataa kukusikiliza, watakapozigeukia njia zao wenyewe, wakiacha kusikia ukweli, jua kuna tatizo, akiacha kukusikiliza ni hatari sana jua kuna rushwa. Ukiona anaacha kukusikiliza kaa tayari” alisema.
Mchungaji huyo aliendelea kuhubiri na kusema ni marufuku kumuhukumu mtu kabla ya kumsikiliza. “Hao ndiyo marafiki wanafiki.Nao wakajiepusha wasisikie yaliyo kweli na watageukia hadithi za uongo. Uongo ukisemwa sana hubadilika na kuwa ni kweli.
“Wale wazee wa Israel walitunga uongo, na wakatoa fedha uongo usambazwe, ule uongo mpaka leo bado unaitafuna Israel.” alisema Mzee wa Upako.
Kabla ya Lusekelo kuingia kanisani, mchungaji mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana alisimama madhabahuni na kusema mwaka huu mwanzoni Mchungaji aliziombea bahasha na kuubariki kuwa mwaka wa kucheka. “Kuna watu wanaotaka kuuharibu, lakini hawatafanikiwa.” “Zimebaki siku 40 kabla ya kumaliza mwaka wa kucheka, lakini kuna watu lazima muwe nao makini wanaweza kusababisha mwaka wa kucheka usiishe vizuri.” alisema
#NIPASHE Kauli ya Rais Magufuli imedaiwa kuweka shakani kazi za wakurugenzi wa TRA na Elimu pia itagusa watendaji wa kata mbalimbali nchini pic.twitter.com/gElwLBNs9Y
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#JAMBILEO Pamoja na kupingwa na wanaharakati, Rais Magufuli ameunga mkono juhudi za RC wa DSM na kueleza yuko naye kwa 100% kwenye kila kitu pic.twitter.com/Pn2bJxnR6s
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#MWANANCHI Gavana wa BOT Benno Ndulu amesema hakuna hasara kiuchumi kuweka fedha kwenye akaunti maalumu kutegemea na malengo yaliyokusudiwa pic.twitter.com/NMk1SH4Qis
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#MWANANCHI Upasuaji ktk mguu wa James Mbatia MB umetumia saa 4 kwenye Hospital ya Zydus Gujarat India, anatarajia kurejea nchini wiki ijayo pic.twitter.com/RwCwNegoGv
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#JAMBOLEO Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA Nicolas Mgaya ameangushwa ktk nafasi hiyo na Dr. Yahaya Msigwa
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#JAMBOLEO Star wa BongoFlava Tundaman amesema amejitoa TIP TOP Connection akidai Meneja Babu Tale amemtelekeza kwa miaka minne bila msaada pic.twitter.com/f3zxnlxI81
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#MWANASPOTI Kipa wa Simba Manyika Peter amesema amevunja uhusiano na mpenzi wake ili kuboresha uwezo wake ulioshuka kwa kuendekeza anasa pic.twitter.com/FfQGWg7YZO
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#NIPASHE Mwanafunzi anayedaiwa kupewa ujauzito na mwalimu wa shule ya Msingi Ilindi wilayani Bahi ameomba serikali imruhusu kusoma sekondari pic.twitter.com/BShdMEPha6
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
#NIPASHE Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI inakabiliwa na kero ya kukatika umeme wakati wa upasuaji na kuhatarisha maisha ya wagonjwa pic.twitter.com/ogFUHELSSz
— millardayo (@millardayo) November 26, 2016
VIDEO: Alice Tupa amekuchambulia Magazeti yote ya leo November 26, 2016. Bonyeza hapa chini kutazama.