Presha ya dirisha dogo la usajili la mwezi January barani Ulaya bado halijafunguliwa lakini vilabu vya soka barani humo vimeshaanza presha ya usajili, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England timu ya Leicester City wameripotiwa kuanza kumuhitaji nyota wa KRC Genk.
Leicester City wanatajwa kuwa mstari wa mbele kumuhitaji beki wa kimataifa wa Nigeria anayeichezea KRC Genk Wilfred Ndindi, Leicester wameripotiwa na 101greatgoals na The Guardian kufikia makubaliano ya kumsajili staa huyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi January 2017.
Leicester City wanamuhitaji Ndindi na watalazimika kulipa pound milioni 15 kwa KRC Genk ili kumpata nyota huyo ambapo Man United wanadaiwa kumuhitaji pia.
VIDEO: Magoli ya Samatta aliyoifungia KRC Genk vs Waasland-Beveren, Nov 30 2016
https://youtu.be/gHHgKqH4ato