Kesi iliyofunguliwa na Bodi ya wadhamini CUF dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Profesa Ibrahimu Lipumba na wanachama 11 wa chama hicho imesikilizwa leo December 6 2016 mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Wakili wa bodi ya wadhamini CUF, Juma Nassoro amesema Jaji anayesimamia kesi, Jaji Kihiyo ajiondoe kwenye kesi hiyo huku akitaja hoja kuu mbili, ya kwanza amesema inajengwa na kesi hiyo wakati ilipotajwa Novemba 11, mwaka huu ambapo Jaji Kihiyo aliibua hoja iliyohusu uhalali wa wadhamini ambayo ilikuwa na muelekeo wa kuwaonyesha wadaiwa nini wafanye.
Aidha hoja nyingine ni kauli iliyotolewa na Jaji huyo kwamba shauri hilo limefunguliwa kwa haraka haraka. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Sakieti Kihiyo anatarajia kutoa uamuzi wa kujitoa ama kutojitoa kuendelea kuisikiliza kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Baraza la Wadhamini la Chama cha Wananchi ‘CUF’, Desember 14, mwaka huu.
VIDEO: Mapokezi ya Prof Lipumba ofisi ya makao makuu ya CUF Buguruni, Bonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: Maalim Seif ana ugomvi na Prof. Lipumba?, Bonyeza Play hapa chini kutazama