December 7 2016 mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano la watu wenye ulemavu nchini ambapo katika hotuba yake aliwataka walemavu kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa ili kujikwamua kiuchumi huku akiahidi kuwasaidia mahitaji mbalimbali zikiwemo ofisi za kudumu.
‘Rais Magufuli ameagiza kila mpango utaofanyika katika ujio wa makao makuu haswa katika maeneo ya fursa ni lazima walemavu wahusishwe, hili litakuwa na maana kwenu endapo litawakuta tayari mmejipanga vizuri katika vyama vyenu‘ –RC Rugimbana
‘Mimi kama mkuu wa mkoa niwahakikishie kuwa hakuna shughuli itayotengwa zikiwemo biashara bila kuwahusisha walemavu, jambo muhimu pia ni lazima kama walemavu muwe na maeneo yanayotambulika zikiwemo ofisi za kudumu‘ –RC Rugimbana
‘Nawaagiza halmashauri zote katika mkoa wa Dodoma kuanzia sasa zihakikishe katika mipango yao zinawafikia makundi ya walemavu na nitalifuatilia, Rais ameonyesha njia na nilazima sisi sote tuitumie hii kama fursa katika kujikwamua kiuchumi‘ –RC Rugimbana
‘Wako wanaofikiri nazungumza maneno kama utani, mimi huwa sitanii na nina mfumo wangu katika utendaji kwahiyo haya yote niliyoahidi mkiona hayafanyiki mwambieni Rais aniondoe lakini kabla sijaondoka wataanza walio chini yangu‘ –RC Rugimbana
Unaweza kuendelea kumsikiliza RC Jordan Rugimbana kwenye hii video hapa chini….
Mambo ya kufahamu kwenye mpango wa Dodoma kuwa jiji