Leo December 15 2016 mkuu wa mkoa wan Dar es salaam, Paul Makonda amefanya ziara katika soko la kariakoo ili kusikiliza na kujibu kero mbalimbali za wafanyabiashara wa soko hilo. Nimekuwekea hapa baadhi ya yaliyojiri kwenye ziara hiyo.
Wafanyabiashara soko la kariakoo wanalalamika kutozwa kiwango kikubwa cha ushuru cha sh 10,000 kwa siku na wengine 25,000 kwa siku #DarMPYA pic.twitter.com/Qqir6ZfQAi
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Soko lilitengenezwa kwa ajili ya mazao lakini soko limebadilika linauza bidhaa za viwanda' ;-RC Makonda #DarMPYA #SokoKARIAKOO pic.twitter.com/eeL4Ah4Nd2
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Viongozi wetu wanaosimamia soko wameonyesha namna soko linavyojiendesha bila kutengeneza faida' RC Makonda #DarMPYA #SokoKARIAKOO pic.twitter.com/VvoPYrJxxz
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Sijaridhishwa na mwenendo wa watu wanaotuwakilisha kwenye soko la kariakoo'- RC Makonda #DarMPYA #SokoKARIAKOO pic.twitter.com/hIY3fG5mhk
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Nataka uchunguzi ufanyike kujua vyanzo vyote vya mapato ya soko la kariakoo'- RC Makonda #DarMPYA #SokoKARIAKOO pic.twitter.com/PAXlcQ3Tet
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Nataka kifanyike kikao cha wanahisa soko la kariakoo, wapitie upya utaratibu wa kupata maeneo na viwango vya ushuru'- RC Makonda #DarMPYA pic.twitter.com/92VOBa1JY3
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Naagiza ufanyike uhakiki inawezekana tukakuta watumishi hewa ndani ya soko la kariakoo' -RC Makonda #DarMPYA #SokoKARIKAOO pic.twitter.com/G2MdX5TAtW
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Wafanyabiashara wanaohujumu maeneo kwa kuwa na vizimba zaidi ya 10 na kazi ni kukusanya kodi wajiandae kuviachia'-RC Makonda #SokoKARIAKOO pic.twitter.com/F7VS4DnYRL
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Tunaenda kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwa kufanya machinga waliokuwa wanauza nguo mtaani wafikie hatua ya kumiliki viwanda vidogo'-Makonda pic.twitter.com/P5pajcBYiF
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Tunaunda uongozi wa mpito wa machinga DSM, tunataka umoja utakaoondoa adha na dhuluma'- RC Makonda #MtaawaCONGO #DarMPYA pic.twitter.com/n7kzjLAxX5
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Sisi tulikuwa tunafukuzana na ninyi machinga ila kwa mapenzi makubwa aliyonayo Rais amekubali hata kubaki peke yake awatetee ninyi'-Makonda pic.twitter.com/66Trq17142
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
RC Makonda amehoji sh 10,000 inayotolewa kwa ajili ya kitambulisho cha wafanyabiashara kariakoo na fomu 5,000, hakilingani na thamani hiyo pic.twitter.com/SuUD7MkLJC
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Namna pekee ya kuonyesha tunampenda Rais ni nyie machinga kufikia hatua ya kumiliki viwanda vidogovidogo'-RC Makonda #DarMPYA pic.twitter.com/zon81NmcaH
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Wakipatikana machinga laki moja tukawa tunachangia kiasi fulani cha fedha inawezekana, saccos ikikamilika nitawachangia mil 100'-Makonda pic.twitter.com/dZTNhqFhm4
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Pale uwanja wa fisi tunataka tuwe na viwanda vidogovidogo, nyie wamachinga natamani muwe pale na viwanda vidogovidogo'-Makonda #Kariakoo pic.twitter.com/Sbct2Vh5SN
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Wamachinga tumuunge mkono Rais wetu kwa kuingia kwenye viwanda, tuanze na viwanda vidogovidogo'-RC Makonda #DarMPYA #Kariakoo pic.twitter.com/ENGoQtL5Ib
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Ifike hatua machinga tuone ufahari kubeba na kuuza bidhaa za watanzania wenzetu, tukifanya hivyo tutapiga hatua'-RC Makonda #Kariakoo pic.twitter.com/i3GSq8ABLi
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
'Wageni waliokuja Tanzania wasifanye kazi ya umachinga, wageni wote badilisheni biashara'-RC Makonda #Kariakoo #DarMPYA pic.twitter.com/MBZNR6kIqm
— millardayo (@millardayo) December 15, 2016
VIDEO: RC Makonda alivyozindua ujenzi wa barabara kwa kuendesha Greda mwenyewe, Bonyeza play hapa chini kutazama
Ulikosa? RC Makonda alivyoamuru wenyeviti watano kuchukuliwa na polisi katikati ya mkutano, Bonyeza play hapa chini kutazama