Leo December 15 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefanya ziara kwenye soko la kariakoo ili kusikiliza na kujibu kero mbalimbali za wafanyabiashara wa soko hilo.
Moja ya kero iliyoibuliwa na wafanyabiashara hao ni pamoja na gharama wanayotozwa kwenye kupata vitambulisho. Wafanyabiashara wamedai kuwa fomu ya maombi wanatozwa 5,000 na kitambulisho wanachopatiwa ni sh 10,000 jumla 15,000.
Baada ya malalamiko hayo RC Makonda aliomba aoneshwe moja ya kitambulisho ambacho kinatolewa na alipopatiwa alihoji kwa mmoja wa kiongozi wa soko hilo kuhusu hadhi ya kitambulisho hicho ikilinganishwa na kiasi cha fedha kinachotolewa. Bonyeza play hapa chini kutazama.
VIDEO: RC Makonda alivyohoji uendeshaji wa soko la kariakoo DSM, Bonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: RC Makonda kuhusu watu wanaohujumu wengine maeneo ya biashara kariakoo, Bonyeza play hapa chini kutazama