Ikiwa ni siku chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuagiza kuwa wamachinga wasisumbuliwe mpaka watakapotengenezewa utaratibu na maeneo ya kufanyia biashara zao.
Leo December 15 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefanya ziara mtaa wa Congo Kariakoo ambao kuna idadi kubwa ya wamachinga wanaofanya biashara eneo hilo.
RC Makonda alisikiliza na kujibu kero mbalimbali ambazo wafanyabiashara hao wanakabiliana nazo na akaelezea mpango wake kuhusu machinga. RC Makonda amesema mpango alionao ni kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwa kufanya wamachinga waliokuwa wanauza nguo mtaani wafikie hatua ya kumiliki viwanda vidogo.
Mpango huo anasema utafikiwa endapo wamachinga watatengeneza umoja wao ambao utakuwa na viongozi na watakuwa wanafanya maamuzi kwa manufaa ya wamachinga wote na si maslahi ya mtu mmojammoja.
RC Makonda anasema anatamani ifike hatua wamachinga watoke kwenye kuuza tu vitu barabarani wafikie hatua ya kumiliki viwanda vidogovidogo na hilo linawezekana endapo kutakuwa na umoja. RC Makonda anasema……
‘Machinga laki moja mkichanga sh 20,000 kwa mwezi mtakuwa na bilioni 2, hapo hatuwezi kuanza hata na kiwanda kimoja’
VIDEO: ‘Hivi kweli hiki kitambulisho kina thamani ya sh 10,000?’-RC Makonda, Bonyeza play hapa chini kutazama
ULIKOSA? RC Makonda alivyoamuru Wenyeviti watano kuchukuliwa na polisi katikati ya mkutano, Bonyeza play hapa chini kutazama